1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHAZNI:Hatima ya mateka 21 raia wa Korea Kusini haijulikani

8 Agosti 2007

Hatima ya mateka 21 raia wa Korea Kusini wanaoshikiliwa na kundi la Taliban nchini Afghanistan bado haijulikani.

Msemaji wa Taliban amesema kwamba kundi lake liko tayari kuwaachilia mateka wanawake kwa sharti kwamba idadi sawa ya wafungwa wanawake wafuasi wa Taliban waachiwe huru.

Gavana wa jimbo la Ghazni amefahamisha kuwa wanamgambo wa Taliban bado wanajadiliana na wawakilishi wa Korea Kusini juu ya mahala pa kufanyia mazungumzo.

Raia 23 wafanyakazi wa shirika la kutoa misaada walitekwa nyara walipokuwa njiani kutoka mji mkuu wa Kabul kuelekea jimbo la kusini la Kandahar wiki tatu zilizopita.

Wawili kati ya mateka hao wameshauwawa.

Wakati huo huo hatma ya mhandisi raia wa Ujerumani aliyetekwa nyara huko huko nchini Afghanistan bado haijulikani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW