1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Vita vimeudhoofisha mfumo wa afya Ukanda wa Gaza

10 Desemba 2023

Mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema vita kati ya Israel na Palestina, vimeathiri pakubwa sekta ya afya katika ukanda wa Gaza.

Ukanda wa Gaza |  Timu ya madaktari wa WHO katika hositali ya Al Shifa
Timu ya madaktari wa WHO lilipotembelea Ukanda wa GazaPicha: WHO/REUTERS

Ghebreyesus ameitisha mkutano maalum wa shirika hilo kujadili hali ya kiafya katika maeneo ya Palestina, akielezea kuporomoka kwa mfumo wa afya huko huku madaktari wakikwamishwa katika shughuli zao.

Mkuu huyo wa WHO amesema watu zaidi wanaendelea kukusanyika katika maeneo madogo, kwahiyo mkusanyiko huo pamoja na ukosefu chakula, maji, makaazi na maeneo masafi ni hatari na huenda vikasababisha hali ya kuenea kwa magonjwa.

Soma zaidi: WHO yaitaja hospitali ya Al Shifa kama "eneo la kifo"

Kwa sasa kuna vitanda 1,400 vya wagonjwa kati ya 3,500 vilivyokuwepo awali, huku hospitali tatu mjini Gaza zikifanya kazi mara tatu ya uwezo wake, bila vifaa vya kutosha vya kufanyia kazi na vile vile kutoa hifadhi kwa maelfu ya watu waliopoteza makaazi yao.

Soma zaidi: WHO kuanzisha hospitali katika Ukanda wa Gaza

Israel imeapa kuendelea na mashambulizi yake dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas lililoanzisha uvamizi nchini Israel mnamo Oktoba 7 na kusababisha mgogoro mkubwa unaoshuhudiwa katika eneo la Mashariki ya Kati.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW