1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO lazima iwe muhimili kushughulikia afya duniani

Hawa Bihoga
23 Mei 2022

Mkuu wa shirika la Afya ulimwenguni WHO Tedros Ghebreyesus,alisema lazima shirika hilo liwe muhimili wa kushughulikia changamoto za kiafya duniani huku akitambua haja ya kufanyika mageuzi ya kimfumo.

WHO Generaldirektor Tedros Adhanom Ghebreyesus
Picha: Fabrice Coffrini/KEYSTONE/picture alliance

Aliyasema hayo katika mkutano wa kwanza wa ana kwa ana baada ya miaka takriban mitatu ya janga la virusi vya Corona kuikumba dunia.

Katika mkutano huo ambao WHO inaibainisha jukumu lake kwa mataifa wananchama kadhalika malengo yake ya baadae uligubikwa na ajenda kadhaa ikiwemo  janga la Corona ambalo limesababisha vifo vya takriban watu milioni 15.

Tedros  Ghebreyesus katika hotuba yake alisema wanahitaji kuwa na shirika la afya ambalo ni madhubuti na lenye ufadhili endelevu, huku likiwa ni muhimili imara wa afya kwa mataifa wananchama.

Gebreyesus aliyasema hayo ikiwa janga la virusi vya Corona linatajwa kuwa lilionesha mianya ambayo shirika hilo linapaswa kushughulikia ili kuimarisha mifumo yake ya kutoa huduma kwa mataifa.

Aliongeza kwamba Miito imekuwa ni mingi katika kushughulikia changamoto za ndani zilizoonesha kuna haja ya mabadiliko ya kimfumo kufanyika kwa haraka iwezekanavyo.

Je umeweza vipi kukabiliana na janga la COVID-19?

03:27

This browser does not support the video element.

Soma zaidi:WHO: Ugonjwa wa homa ya ini umewapata takriban watoto 200

Hii ni baada ya jopo huru kuueleza mkutano huo kwamba WHO haikuwa na uwezo madhubuti wa kuchunguza mlipuko na kuratibu hatua za kuzuia wakati wa Uviko 19.

Mataifa wanachama 194  yalionekana kugawanyika ikiwa shirika hilo linastahili mabadiliko mapya kutokana na namna ambavyo limeshughulikia janga la Corona.

Hata hivyo Gebreyesus alisisitiza katika hotuba yake hawakujiandaa na wala hawajajiandaa.

" sasa kwa kazi yetu ya dharura ni wazi kwamba dunia haikuwa na bado haijajiandaa kwa janga "

Taiwan yazuiliwa kuhudhuria mkutano huo muhimu

Mongoni mwa mambo mengine yalioangaliwa zaidi katika mkutano huo ni pamoja na tangazo la Rais wa barazahilo la mawaziri wa afya ambae pia ni waziri wa afya Djibouti Ahmed Robleh Abdilleh, alisema Taiwan haijajumuishwa kushiriki mkutano huo kama taifa huru, kutokana na shinikizo la Beijin kushikilia msimamo wake kwamba kisiwa hicho ni sehemu ya ardhi yake.Soma zaidi:Tedros: Mizozo mingine duniani yabezwa, kisa wanaoteseka si weupe

wakaazi wa Taiwan wakiwa wamevalia barakoa kujikinga na CoronaPicha: Chiang Ying-ying/AP/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan imeonesha kusikitishwa na kutoridhishwa na uamuzi huo na kusema kwenye taarifa yake kwamba matumizi ya siasa za kujirudia ya China kubadilisha maslahi ya umma,afya,kukandamiza haki za watu wa Taiwan haikubaliki.

Hata hivyo mataifa makubwa kama vile Marekani na Uingereza yamekuwa yakionesha ushirikiano wa karibu na Taiwan.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW