1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoAustralia

FIFA yasema wachezaji watalipwa na mashirikisho ya nchi zao

20 Julai 2023

Mashindano ya Kombe la Dunia ya Wanawake kea mara ya kwanza yauza haki ya biashara ya matangazo kwa kutenganishwa na yale ya wanaume ingawa bado mfuko wa fedha bado uko chini.

Schweiz Genf | FIFA Präsident Gianni Infantinos
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino akizungumza katika mjadala wa soka la wanawake mjini Geneva.Picha: Fabrice Coffrini/AFP

  
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameshindwa kuweka wazi kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani litawalipa kiasi cha dola za kimarekani 30,000 zilizoahidiwa kwa kila mchezaji kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Wanawake yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho na kwamba watalipwa na mashirikisho wanachama.

Soma zaidi: Mashindano mapya ya Kombe la Dunia la FIFA ngazi ya klabu kufanyika sambamba na CONCACAF

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya ufunguzi wa mashindano hayo akishirikiana na mashirikisho ya wanachama ameeleza kuwa malipo hufanywa na mashirikisho ya kitaifa na hivyo hata malipo haya yanatarajiwa kulipwa kwa  wachezaji  kwa namna hiyo na bado hakuna utaratibu wa kuwalipa wachezaji moja kwa moja pesa hizo ambazo baadhi ya wadau wanakiri kwamba zingeweza kubadili kabisa maisha ya wachezaji.

Wachezaji wa timu ya wanawake ya Marekani wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho mwisho kuelekea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake huko Auckland, New Zealand:Picha: Alan Lee/Action Plus/IMAGO

Malipo yatafanywa na mashirikisho ya nchi zao.

Infantino amesema "Tunasonga bila shaka katika mwelekeo sahihi, tumekuwa
tukishauriana na vyama, na wachezaji, kujaribu kwenda katika njia ya haki," 

Infantino ameongeza na kusema, "Tumetoa mapendekezo haya, lakini sisi
kuwa na muungano wa vyama. Kwa hivyo malipo yoyote tunayofanya, sisi
itapitia vyama na kisha vyama vitafanya  malipo husika kwa wachezaji wao wenyewe. Tuna ukaribu na tunawasiliana na vyama vyote."

Soma zaidi: FIFA yazindua vitambaa vya kutetea haki kombe la dunia la wanawake

FIFA hapo awali ilithibitisha kuwa wachezaji 732 watakaoshiriki 
Kombe la Dunia kila mmoja atalipwa kiasi cha dola za kimarekani 30,000 kila moja. Na malipo yatakuwa yanaongezeka ikiwa timu itafanya vizuri kwa kila mchezaji na kwa timu itakayoshinda itapata kiasi cha dola 270,000.

Infantino amesema kwamba sababu kubwa ya kufanya hivo ni kwamba kuna matatizo katika masuala ya makaazi na kodi kwa hivyo ni vyema yakishughulikiwa vyema na mashirikisho wanachama.
Rais huyo ameongeza  msisitizo kwamba malipo ni muhimu kwa wachezaji na  wastani wa kila mwaka mshahara duniani kote kwa wanawake wanaocheza soka la kulipwa ni dola 14,000 huku makubaliano ya FIFA yanamaanisha nusu ya pesa zote za tuzo za Kombe la Dunia za mfuko wa dola milioni 110 utalipwa kwa wachezaji katika timu 32. 

Mashindano ya mwaka huu yako tofauti na yale yaliyofanyika mwaka 2019, mfano zawadi kwa mshindi wa mwaka huu atapata zaidi ya mara tatu ya mfuko wa tuzo wa FIFA wa dola milioni 30 iliyolipwa kwenye Kombe la Dunia la Wanawake la 2019 nchini Ufaransa.

Soma zaidi: Kombe la Dunia la Wanawake kuanza kutimua vumbi

Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani wakimpigia makofi mmoja wa watu wanaocheza mchezo wa didgeridoo huko Australia wakati wa mazoezi ya kujiandaa na Kombe la Dunia kwa Wanawake.Picha: Dean Lewins/AAP/IMAGO

Muungano wa wachezaji wa kimataifa, unaojulikana kama FIFPRO, umekuwa ukiihimiza  FIFA kutoa asilimia ya pesa za tuzo kwa wachezaji wenyewe na sio kuzipeleka katika mashirikisho yao.  Mwezi Oktaba mwaka uliopita muungano huo ulituma barua kwa FIFA kwa niaba ya wachezaji kutoka timu 25 za kitaifa zinazotoa wito kwa masharti ya usawa zaidi wa  zawadi ya pesa.

Uwiano wa fedha bado haulinagani.

Hata hivyo, mfuko wa pesa za tuzo za Kombe la Dunia kwa Wanawake  bado uko chini ya dola milioni 440 zinazolipwa kwa wanaume waliocheza Kombe la Dunia mwaka jana nchini Qatar ingawa Infantino ameeleza kwamba  lengo ni kusawazisha pesa za tuzo ifikapo 2026.

Infantino amegusia pia mapato yatakayopatikana kwenye Kombe la Dunia la Wanawake linaloanza hapo kesho kuwa ni  dola nusu bilioni. Mashindano haya kwa mara ya kwanza yameuza haki ya kibiashara za matangazo kwa kutenganishwa na zile za mashindano ya wanaume.

Mashindano hayo yanafunguliwa siku ya Alhamisi huku waandaji wenza wote wawili wakishiriki katika mechi za ufunguzi. New Zealand itacheza na Norway huko Auckland, na Australia itamenyana Ireland huko Sydney.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW