GLASGOW: Sevilla tena yashinda kombe la UEFA
17 Mei 2007Matangazo
Barani Ulaya klabu ya Sevilla imeshinda kombe la kandanda la UEFA kwa mara ya pili kwa mfululizo baada ya kuifunga Espanyol katika fainali ya kupiga mabao baada ya mahasimu hao kwenda sare mabao 2-2 mjini Glasgow.Katika penalti kipa wa Sevilla alizuia mikwaju mitatu na amekuwa mbabe wa klabu yake.