1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GLENEAGLES: Afrika kuongezewa msaada

8 Julai 2005

Viongozi wa nchi tajiri 8 duniani wamekubaliana kuongeza fedha za msaada wa maendeleo kwa ajili ya nchi za Afrika na kuzifutia madeni nchi hizo.

Nchi tajiri zitaongeza dola bilioni 50 kila mwaka hadi kufikia mwaka wa 2010.

Bara la Afrika litatengewa dola bilioni 25 kila mwaka.

Mataifa tajiri pia yamekubaliana kusamehe madeni ya nchi 14 za Africa.

Viongozi wa nchi hizo waliomaliza mkutano wao leo nchini Scotland pia wameafikiana juu ya kuanza mazungumzo juu ya kulikabili tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW