1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GMF: Kuchangiana Masuluhisho dunia inapokabiliwa na migogo

17 Juni 2024

Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari linaloandaliwa na DW limeanza leo mjini Bonn, likiwa na mada kuu "Kuchangiana Masuluhisho", ambapo wanahabari wanasaka majibu kwenye ulimwengu uliotawaliwa na migogoro.

GMF 2024 | Keynote Annalena Baerbock
Picha: Björn Kietzmann/DW

Washiriki zaidi ya 1,500, wazungumzaji zaidi ya 160, kutoka nchi zaidi ya 100 ndani ya siku mbili hapa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano mjini Bonn.

Wote wanajaribu kusaka njia za kushirikiana kukabiliana na ulimwengu unaozama kwa kasi kwenye migogoro, iwe ya vita, mabadiliko ya tabianchi na, kwa siku za karibuni, teknolojia mpya ya akili ya kubuni, ama kama waiitavyo wengine, akili mnemba.

Katikati ya migogoro hiyo, ni jukumu la wanahabari kuunganisha baina ya makundi mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kijinsia, ili kuufanya ulimwengu kuwa mahala salama kwa kuishi kwa kila mmoja.

Soma pia:Kongamano la vyombo vya habari la DW kuangazia usumbufu na ubunifu

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Bearbock, amesema kwenye hotuba yake kwa washiriki kwamba hiyo ndiyo nguvu ya vyombo vya habari:

"Nguvu kubwa kabisa ya uandishi wa habari, ya nyinyi nyote muliopo hapa leo, ni uwezo wa kusimulia hadithi ambazo kama si nyinyi kamwe zisingejuilikana, kuuliza maswali ambayo kama si nyinyi kamwe yasingejibiwa, kuwawajibisha wale ambao nguvu zao kama si nyinyi huwa hazihojiwi, na kuwapa sauti wale ambao kama si nyinyi wasingesikika."

Uwandishi wa habari wenye kuleta matokeo

Mbali ya maudhui makuu ya Kuchangiana Masululisho, ambayo lengo lake ni kukusanya mawazo ya kila mmoja kwenye kutatua matatizo yanayotukabili, kongamano hili pia linajadili kile kinachoitwa uandishi habari wa kujenga, mbinu za kuripoti kwenye maeneo ya migogoro mikubwa ya kisiasa na kijamii, na pia nafasi ya teknolojia ya akili ya kubuni, ambayo kwa sasa inakuwa kwa kasi kwenye ulimwengu wa mawasiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa DW Peter Limbourg akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock.Picha: Philipp Böll/DW

Antony Diallo ni mdau wa tasnia ya habari na mwanasiasa wa siku nyingi nchini Tanzania, ambaye ana wasiwasi na jinsi ambavyo teknolojia hiyo inavyotumika kwenye vyombo vya habari:

Kongamano hili ni fursa ya wanahabari kukutana kutoka pande mbalimbali ulimwenguni, kuanzisha mawasiliano na kubadilishana uzoefu kwenye taaluma yao.

Soma pia:Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari laanza Bonn

Ndio maana mbali ya waandishi wakubwa wa kimataifa, Deutsche Welle huwaalika pia waandishi kutoka jamii za pembezoni, na makundi yasiyo na sauti, kama vile wakimbizi.

Nira Ismail, mwanahabari kutokea kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, mwenyewe akiwa mkimbizi kutokea Sudan

"Hakuna haja ya mwandishi kutoka taifa jingine aje kuzungumza kwa niaba yetu laah! Wenyewe tunaweza kujizungumzia na kupata masuluhisho."

Kongamano linaendelea na kumalizika kesho, ambapo washiriki wanatarajiwa kuendeleza mjadala mzito ulioanzia leo juu ya dhima ya vyombo  vya habari vya mataifa ya kusini, yaani mataifa masikini, yanayolalamika kuwa hadithi yake inasimuliwa vibaya na vyombo vya habari vya kaskazini, kwa maana ya mataifa tajiri.

Kongamano la vyombo vya habari laanza Bonn Ujerumani

02:35

This browser does not support the video element.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW