1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Goma, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Nkunda atangaza vita na majeshi ya serikali.

9 Oktoba 2007

Kiongozi wa waasi katika eneo la mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo DRC ametangaza kuwa majeshi yake yatafanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali. Jenerali huyo muasi Laurent Nkunda amesema kuwa wapiganaji wake waasi wametupilia mbali makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja nchini DRC. Mapigano mapya yalizuka siku ya Alhamis na yanaendelea hadi leo.