GOMA : Kabila aamuru waasi kunyanganywa silaha
18 Oktoba 2007Matangazo
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Joseph Kabila hapo jana ameamuru vikosi vyake kujiandaa kuwanyanganya silaha wapiganaji 5,000 wa Generali muasi Laurent Nkunda.
Kabila akiwa kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini wa Goma amesema makao ya kijeshi yamepewa ruhusa kuanza kujiandaa kuwanyanganya silaha ikibidi hata kwa kutumia nguvu kwa Nkunda na wale wote walioko naye.
Kabila ameuambia mkutano wa waandishi wa habari baada ya zaidi ya mwezi mmoja wa mapambano kwenye jimbo hilo kati ya jeshi la serikali na waasi wa Nkunda kwamba Bw.Nkunda ni mhalifu na kumekuwepo hati ya kukamatwa kwake.