1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Greenland ina uungwaji mkono thabiti wa Umoja wa Ulaya

8 Januari 2026

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Antonio Costa, amesema kuwa Umoja wa Ulaya utaiunga mkono Greenland na Denmark inapohitajika na hautakubali ukiukaji wa sheria za kimataifa popote pale unapotokea.

Ubelgiji Brussels 2025 | Antonio Costa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya.
Antonio Costa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya.Picha: Stephanie Lecocq/REUTERS

Akizunguma katika hotuba ya kuashiria kuanza kwa Cyprus kushika urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya amesema hakuna kitu kinachoweza kuamuliwa kuhusu Greenland bila Denmark. Na kuongeza kuwa watu wa eneo hilo "Wana uungwaji mkono kamili na mshikamano wa Umoja wa Ulaya." Katika siku za hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani, amekuwa akirejea kauli ya kwamba anataka kuichukua Greenland, akidai kisiwa hicho ni muhimu kwa mkakati wa kijeshi wa Marekani na akisema Denmark haijafanya vya kutosha kukilinda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW