1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Griezmann astaafu timu ya taifa

30 Septemba 2024

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann ametangaza kustaafu kwake kutoka kwenye kandanda la kimataifa.

EURO 2024 Ufaransa vs Uhispania
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Antopine GriezmannPicha: Annegret Hilse/REUTERS

Griezmann ambaye alikuwa na wakati mgumu katika mashindano ya kuuwania ubingwa wa Ulaya mwaka huu hapa Ujerumani, alikuwa nguzo ya Ufaransa katika miaka iliyopita ambapo walinyakua ubingwa wa dunia katika Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 na walipomaliza wa pili katika mashindano hayo hayo huko Qatar.

Griezmann mwenye umri wa miaka 33 anasema wakati umewadia kwake kutoa nafasi kwa wachezaji wachanga konyesha uwezo wao.

Chanzo: Reuters/AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW