GUANGZHOU:Nigeria kuongeza viwanda vya kutengeza dawa
17 Januari 2007Nigeria iko katika hatua za mwisho za kupitisha sheria itakayoruhusu watengezaji dawa kutengeza dawa zaidi ili kupambana na magonjwa ya Malaria na Ukimwi.Nchi hiyo ina kampuni 14 za kutengeza dawa za kupunguza makali ya Ukimwi na mengine manane ya kutengeza dawa aina ya artemisinin za kutibu Malaria.Hayo ni kwa mujibu wa mshauri maalum wa Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria Ahmed Abdulkadir anayeongoza mpango maalum wa kushughulikia suala hilo akiwa mjini Guangzhou nchini Uchina.
Takriban watu milioni 2 u nusu na 3 wana virusi vya HIV na Ukimwi.Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni WHO zinaonyesha kuwa malaria huathiri takriban watu milioni tano kila mwaka na kusababisha vifo vya zaidi yaw engine milioni moja.Vifo vingi vinatokea katika eneo lililo kusini mwa jangwa la Sahara.