1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea Bissau. Uchaguzi wa marudio wamalizika Guinnea Bissau.

25 Julai 2005

Uchaguzi umemalizika katika uchaguzi wa marudio wa kumchagua rais mpya katika taifa hili la Afrika magharibi la Guinea – Bissau. Uchaguzi uliofanyika jana Jumapili ulikuwa kati ya marais wawili wa zamani , mgombea wa chama tawala Malam Bacai Sanha na mgombea wa kujitegemea Joao Bernardo Vieira, ambaye miaka yake 19 ya utawala wa kidikteta ilikatishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1999.

Vieira alikimbilia Ureno mkoloni wa zamani wa taifa hilo la Guinea Bissau, na alirejea kutoka uhamishoni kwa kishindo na mapokezi makubwa mwezi wa Aprili.

Uchaguzi huo unakuja siku chache tu baada ya shambulio la watu wenye silaha dhidi ya majengo ya serikali ambapo polisi wawili waliuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa katika muda wa wiki moja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW