1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea-Bissau wapigia kura kuchagua wabunge

Hawa Bihoga
4 Juni 2023

Wapiga kura nchini Guines-Bissau wamepiga kura leo Jumapili kuwachagua wabunge, katika uchaguzi ulioitishwa na rais anaeshinikiza mabadiliko ya katiba baada ya miaka chungu mzima ya kukosekana utulivu katika taifa hilo.

Guinea-Bissau | Palamentswahlen | Präsident Umaro Sissoco Embalo
Picha: DW

Wapiga kura takriban 884,000 wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura kuwachagua wabunge 102, huku waangalizi wa kimataifa wapatao 200 wakifuatilia mchakato huo wa kidemocrasia wakati hali ya usalama ikiimrishwa katika vituo vya kupiga kura.

Vyama zaidi ya 22 vya kisiasa vimejitokeza kushiriki uchaguzi huo ikiwemo chama cha Rais Umaro Sissoco Embalo cha Madem G15.Matokeo yanatarajiwa kutangazwa saa 48, baada ya kutamatishwa kwa upigaji kura.

soma pia:Guinea-Bissau:ECOWAS imelitolea mwito jeshi kubaki kando na siasa

Kufichuliwa kwa jaribio la mapinduzi mapema mwaka uliopita,Rais Embalo alivunja bunge mwezio Mei baada ya kutofautiana na wabunge na kusababisha kuzorota kwa hali ya kisiasa nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW