1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea: Doumbouya atangaza kipindi cha mpito cha miezi 39

Daniel Gakuba
1 Mei 2022

Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kanali Mamady Doumbouya ametangaza kipindi cha miezi 39 cha utawala wa mpito, kabla ya nchi hiyo kurejea katika uongozi wa kiraia, akisema pendekezo la muda huo litawasilishwa bungeni.

Conakry, Guinea | Mamady Doumbouya
Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kanali Mamady Doumbouya ametangaza kipindi cha utawala cha miezi 39 ya utawala wa mpitoPicha: John Wessels/AFP

Tangazo la kiongozi huyo mwanajeshi lilitolewa baada ya kuundwa kwa kile ambacho mamlaka nchini Guinea ''mfumo shirikishi wa mashauriano'' mnamo mwezi Aprili. Mchakato wa kuunda mfumo huo ulimalizika kwa kususiwa na makundi maarufu ya upinzani nchini humo.

Ijumaa iliyopita, baraza la mawaziri linalodhibitiwa na wanajeshi lilisema jukwaa lilioujadili mfumo huo lilitafakari uwezekani wa kuweka kipindi cha uongozi wa mpito cha kati ya miezi 18 na 52. Katika hotuba yake, Kanali Doumbouya amesema muda wa miezi 39 aliouridhia ni ni wastani wa mapendekezo yaliyofikiriwa.

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ilikuwa imeweka Jumatatu iliyopita kama muda wa mwisho kwa serikali ya kijeshi ya Guinea kuwa imetangaza ratiba ya ''inayokubalika'' ya kuondoka katika utawala wa mpito, la sivyo ikabiliwe na vikwazo vya kiuchumi na kifedha.

Alpha Conde, kiongozi wa Guinea aliyeangushwa na wanajeshiPicha: Präsidentschaft der Republik Guinea

Jeshi la Guinea lapuuza muda wa mwisho

Hata hivyo, utawala wa kijeshi mjini Conakry uliuacha muda huo upite, ikiitka ECOWAS kuurefusha ili iweze kuendeleza mashauriano.

Jeshi lilichukua hatamu za uongozi wa Guinea mwezi Septemba 2021, baada ya kuiangush serikali ya Rais Alpha Conde, aliyekuwa amechaguliwa kuongoza muhula wa tatu katika uchaguzi ulioandamwa na utata.   

Conde mwenye umri wa miaka 84 aliukasirisha upinzani kwa kulazimisha mabadiliko y katiba mwaka 2020, ambyo yaliondoa ukomo wa mihula miwili kwa rais na kumruhusu kugombea mara ya tatu.

Baada ya kuangushwa kwake, ECOWAS ilikuwa imewataka watawala wapya kuirejesha nchi hiyo ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa, katika uongozi wa kiraia katika kipindi kisichozidi miezi sita.

Ingawa mwanzoni ri wengi wa Guinea walishangiria kupinduliwa kwa ris Alpha Conde, hivi sasa malalamiko yanaongezeka dhidi ya utawala wa kijeshi. Jeshi la nchi hiyo liliiangusha serikali ya kiraia, muda si mrefu baada ya tukio kama hilo nchini Mali.

Bendera za baadhi ya nchi wanachama wa ECOWAS, jumuiya inyotuhumiwa kuwa na undumilakuwili kuhusiana na vikwazo vyakePicha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Tuhuma za undumilakuwili upnde wa ECOWAS

ECOWAS iliiwekea vikwazo vikali Mali, ikiifunga mipaka yote ya nchi hiyo na majirani zake, ikishikilia fedha zote za nchi hiyo katika Benki Kuu ya ECOWAS, na kusitisha biashara zote kati ya mali na nchi nyingine wanachama.

Kwa upande wa Guinea, ni viongozi waandamizi tu wa kijeshi waliowekewa vikwazo, vinavyojumuisha marufuku ya usafiri katika nchi za ECOWAS.

Burkina Faso, nchi nyingine ya ukanda huo wa Afrika Magharibi iliyoshuhudia pia mapinduzi ya kijeshi mwezi Januari, haikuwekewa vikwazo kama Mali na Guinea, lakini pia ilikuwa imepewa hadi Jumatatu iliyopita kuwa imetangaza tarehe ya uchaguzi.

Wanajeshi walioshika madaraka nchini humo wamesema wanashikilia msimamo wao wa kuandaa uchaguzi baada ya kipindi cha mpito cha miaka mitatu, kwa hoja kwamba inabidi kwanza washughulikie kadhia ya vurugu zinazosababishwa na makundi ya kijihadi yenye silaha.

 

Chanzo: afpe

 

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW