1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea ya Ikweta yathibitisha mripuko wa kwanza wa Marburg

14 Februari 2023

Guinea ya Ikweta imethibitisha mripuko wa kwanza kabisaa wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg.

Marburg-Virus
Picha: CDC/dpa/picture alliance

Waziri wa afya nchini humo amesema jana Jumatatu kwamba watu wasiopungua tisa wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika mkoa wa Kie-Ntem.

Shirika la afya duniani, WHO, pia limethibitisha mripuko huo, na kusema timu za wataalamu zimetumwa kufuatilia watu waliotangamana na waathirika, kuwatenga wale wanaoonesha dalili na kutoa huduma.

Soma pia:Cameroon yaweka vizuizi mkapani na Guinea ya Ikweta

Dalili za ugonjwa huo mpaka sasa zinahusisha uchovu, matapishi yaliochanganyika na damu na kuharisha.

Waziri wa afya Mitoha Ondo'o Ayekaba, amesema tahadhari ya kiafya imetangazwa katika mikoa ya Kie-Ntem na Mongomo.

Kirusi cha Marburg kinahusiana na Ebola, ambayo ilisababisha maafa makubwa katika miripuko kadhaa ya huko nyuma barani Afrika.

Hakuna chanjo zilizoidhinishwa au dawa za kutibu ugonjwa wa Marburg, lakini tiba ya kuongeza maji mwilini kupunguza dalili inaweza kuongeza nafasi ya kupona kwa mgonjwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW