1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea yawaonya watakaochapisha taarifa za uongo

4 Desemba 2024

Serikali ya kijeshi nchini Guinea imeonya kumfunga mtu yoyote atakayechapisha taarifa za uongo na zisizothibitishwa kuhusiana na vifo vya mashabiki wa soka vilivyotokea baada ya mkanyagano.

Mkanyagano umetokea kwenye uwanja kufuatia mapigano kati ya mashabiki wakati wa mechi ya kandanda.
Mkanyagano umetokea kwenye uwanja kufuatia mapigano kati ya mashabiki wakati wa mechi ya kandanda. Picha: Social media via REUTERS

Serikali ya kijeshi nchini Guinea imeonya kumfunga mtu yoyote atakayechapisha taarifa za uongo na zisizothibitishwa kuhusiana na vifo vya mashabiki wa soka vilivyotokea baada ya mkanyagano.

Soma pia: Makumi ya watu wafariki Guinea katika mkanyagano 

Waziri wa Sheria Yaya Kairaba Kaba amesema kwenye video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook jana usiku kwamba kusambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazoweza kuleta usumbufu kwa umma hakuruhusiwi na wanaohusika watachukuliwa hatua.

Kairaba amesema "Kwa mamlaka niliyo nayo kama waziri wa sheria na msingi wa kifungu cha 37 cha Kanuni ya Mwenendo wa Jinai, nimemuagiza Jaji Mkuu, karibu na Mahakama ya Rufaa ya Kankan kuanzisha mara moja uchunguzi wa kimahakama ili kuwawajibisha wahusika wa janga hili na kuwashitaki pamoja na washirika wao."
Kulingana na serikali, watu 56 walikufa siku ya Jumapili kwenye mkanyagano uliosababishwa na maamuzi ya refa, mashabiki kuingia uwanjani na polisi kutumia gesi ya machozi kuwatawanya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW