1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guirassy avunja rekodi za Bundesliga

9 Oktoba 2023

Mshambuliaji wa VfB Stuttgart Serhou Guirassy ameweka rekodi kwa kufunga magoli 13 msimu huu na kuandikisha mwanzo mwema zaidi wa msimu katika historia kwa klabu yake.

Ligi Kuu ya Ujerumani VfB Stuttgart vs VfL Wolfsburg 07 | Serhou Guirassy
Mshambuliaji wa VfB Stuttgart Serhou GuirassyPicha: THOMAS KIENZLE/AFP

Stuttgart ilipokuwa ikicheza na VfL Wolfsburg Jumamosi, Guirassy alifunga mabao yote matatu walipovuna ushindi wa 3-1.

Guirassy ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa ila anaichezea timu ya taifa ya Guinea, amefunga magoli mengi zaidi katika mechi saba kwanza za Ligi Kuu ya Ujerumani kuliko mchezaji mwengine yeyote katika historia ya Bundesliga. Rekodi ya awali ilikuwa mabao 11.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW