1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gurudumu la bembea lajeruhi watu 30 kwenye tamasha Ujerumani

18 Agosti 2024

Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa baada ya gurudumu la bembea kwenye tamasha la Highfield karibu na mji wa mashariki wa Ujerumani wa Leipzig kushika moto Jumamosi jioni kwa mujibu wa polisi.

Leipzig
Gurudumu la bembea likiwa linawaka moto kwenye tamasha lilokuwa linafanyika karibu na mji wa Leipzig nchini UjerumaniPicha: STR/dpa/picture alliance

Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa baada ya gurudumu la bembea kwenye tamasha la Highfield karibu na mji wa mashariki wa Ujerumani wa Leipzig kushika moto Jumamosi jioni kwa mujibu wa polisi.

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa na msemaji wa polisi kwa shirika la habari la dpa ni kwamba waathirika wote walipata changamoto ya kuvuta pumzi kutokana na moshi baada ya bembea hiyo yenye raundi mbili kushika mot

Soma zaidi. Xavi Simons kubakia Leipzig

Mkuu wa operesheni wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Ujerumani, hata hivyo, alisema watu wawili walijeruhiwa vibaya zaidi huku polisi wanne pia wakiwa ni miongoni mwa waliojeruhiwa. Bado chanzo cha moto huo hakijabainika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW