Guterres aelezea aitaka dunia kuachana nishati ya visukuku
17 Januari 2024Matangazo
Akizungumza katika kongamano la kiuchumi la dunia mjini Davos Uswisi, Guterres ameeleza kuwa dunia haina budi kuondokana na matumizi ya nishati ya visukuku na anatumai kuwa, dunia haitochelewa kufanya hivyo.
Takriban mataifa 200 yalikubaliana kwa sauti moja katika mkutano wa kilele wa mazingira wa COP28 mwezi uliopita kuanza kupunguza matumizi ya nishati ya visukukuu ili kuepusha janga baya la mazingira.
COP28 yafikia makubaliano kuachana na nishati za visukuku
Makubaliano hayo, yaliyofikiwa baada ya wiki mbili za mazungumzo, yalikuwa na nia ya kutuma ujumbe kwa wawekezaji na viongozi wa siasa duniani kuachana na nishati ya visukuku.