1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres aelezea wasiwasi wa ongezeko la vurugu Sudan

30 Januari 2026

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wa ongezeko la vurugu nchini Sudan Kusini na amesisitiza wito wake wa kulindwa kwa raia.

Marekani New York 2026 | Antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari
Katibu wa Umoja wa Mataifa, Antonio GuterresPicha: Selcuk Acar/Anadolu Agency/IMAGO

Katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake Stephane Dujarric, Guterres amesema vikosi vya serikali na vya upinzani vinapaswa kuchukua hatua za mara moja na maamuzi ya kusitisha shughuli zote za kijeshi pamoja na kupunguza vurugu hizo kupitia mazungumzo jumuishi.

Matamshi yake yanakuja baada ya jeshi la nchi hiyo kuwaamuru raia na wafanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na mashirika yote ya misaada kuondoka katika kaunti tatu kwenye Jimbo la Jonglei kabla ya kufanyika kwa operesheni dhidi ya vikosi vya upinzani katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW