Guterres aisifia Somalia kuanza kujijenga kitaasisi
21 Mei 2019Matangazo
Hata hivyo, Guterres alisema kuwa inabidi serikali ya Somalia ipambane na watu wenye itikadi kali wanaotumia nguvu, ugaidi, makundi yenye silaha, hali tete ya kisiasa na rushwa.
Aliyasema hayo katika ripoti iliyowasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusambazwa siku ya Jumatatu (Mei 21) kwamba changamoto hizo zinaonesha udhaifu wa hatua zilizopigwa hadi sasa na kutishia maendeleo zaidi.
Baada ya miongo mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mashambulizi ya watu wenye itikadi kali na njaa, Somalia imeweza kuwa na serikali kamili mwaka 2012 na hadi sasa imekuwa ikifanyakazi kujenga hali thabiti.