1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Imetimia miaka miwili tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7

7 Oktoba 2025

Waisrael wanajiandaa kuomboleza waliouawa, wakati taifa hilo linaadhimisha miaka miwili tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7, ambalo liliingiza eneo hilo katika vita vya maangamizi

Marekani New York 2025 | Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika sherehe za kuadhimisha miaka 80 ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo duniani katika makao makuu yake mjini New York Septemba 22, 2025.Picha: Kyodo/picture alliance

Katika kumbukumbu ya miaka miwili tangu mauaji ya Oktoba 7 yaliyofanywa na Kundi la Hamas nchini Israel, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kusitisha vita vya Gaza. Kiongozi huyo amenukuliwa akisisitiza: "Sitisheni uhasama katika Gaza, Israel na eneo lote sasa." Guterres aliongeza kuwa pendekezo jipya la Rais wa Marekani Donald Trump linatoa fursa ya kumaliza mgogoro huo ikiwa ni baada ya miaka miwili ya maumivu, ni lazima kufanikishwe matumaini.Oktoba 7, 2023, wapiganaji wa Hamas na makundi mengine ya Kiislamu walitekeleza mauaji mabaya zaidi katika historia ya Israel, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na zaidi ya 250 kutekwa na kupelekwa Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW