1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres aonya Gaza inaendelea kuteseka 'kila baada ya saa'

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Jumapili ameonya kuwa hali katika Ukanda wa Gaza inayotawaliwa na Hamas inazidi kuzorota kwa kasi,

USA, New York | Guterres auf einer Pressekonferenz im UN Hauptquatier
Guterres amesisitiza umuhimu wa kusitishwa mapigano GazaPicha: Xie E/Xinhua/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Jumapili ameonya kuwa hali katika Ukanda wa Gaza inayotawaliwa na Hamas inazidi kuzorota kwa kasi, huku akirudia ombi la kusitishwa kwa mapigano ili kukomesha kile alichokiita "jinamizi" la umwagaji damu.

Soma pia: Guterres atoa wito wa usitishwaji mapigano Gaza

Gutterres ameyasema hayo akiwa ziarani nchini Nepal na kuongeza kwamba badala ya kusimamisha mashambulizi hoja inayoungwa mkono na jumuiya ya Kimataifa, Israel imezidisha mashambulizi yake ya kijeshi.

Baada ya mashambulizi makubwa ya mabomu kwa majuma kadhaa katika Ukanda wa Gaza, wizara ya afya Palestina imesema watu zaidi 8,000 wameuwawa, huku jeshi la Israel likisema hatua ya pili ya vita imeanza kwa uvamizi wa ardhini tangu Ijumaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW