1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Guterres aonya juu ya sheria ya kuzuia shughuli za UNRWA

9 Oktoba 2024

Antonio Guterres ametahadharisha juu ya kile alichokiita "janga la kibinadamu” kutokana na sheria ya Israel ambayo inaweza kuzuia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kufanya kazi.

Marekani | Umoja wa Mataifa | New York | Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Richard Drew/AP Photo/picture alliance

Katika mkutano na waandishi wa habari, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amemjulisha waziri mkuu Benjamin Netanyahu juu ya rasimu ya sheria katika bunge la Israel ambayo zinaweza kuzuia shirika la UNRWA kuendelea na kazi yake katika ukanda wa Gaza.

Soma pia: Israel yauachia msafara wa wafanyakazi wa UNRWA Gaza 

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema sheria hiyo inaweza kuwa pigo kwa mwitikio wa kimataifa kutoa msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza.

Kamati ya mambo ya nje na ulinzi katika bunge la Israel, Knesset, imeidhinisha miswada miwili ambayo inalenga kusitisha shughuli za shirika la UNRWA nchini Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW