Guterres asema MONUSCO inakaribia kuondoka Kongo
12 Agosti 2023Matangazo
Guterres hata hivyo ametoa tahadhari huwa hali katika taifa hilo lenye mzozo imezorota kwa kasi.
Kupitia ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Guterres alitoa tathmini ya kina juu ya machafuko katika taifa hilo na kutangaza mipango ya kuuondoa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, kwa njia ya haraka lakini isiyoyumbisha usalama.
Ripoti hiyo ya kurasa 15 imeonesha kuwepo kwa ongezeko la mivutano na hali mbaya ya kiutu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakati maelfu ya raia wakilazimika kuyahama makazi yao.
Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa, unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto umeongezeka mara mbili kutoka mwaka 2021 hadi 2022. Maeneo yalioathiriwa zaidi na mzozo huo yametajwa kuwa ni Kivu Kaskazini na Ituri,