Guterres ataka hatua za haraka kuinusuru sayari ya dunia
27 Julai 2023Matangazo
Akizungumza jijini New York, Guterres amesema hali ya joto inayovunja rekodi mwezi Julai inaonesha kwamba dunia imevuuka awamu ya joto na sasa imeingia kile alichokiita enzi ya "kuchemka."
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kumekuwa na msimu hatari wa joto katika eneo la kaskazini mwa dunia kutokana na joto lililopita kiasi.
Soma zaidi: UN:yapitisha azimio muhimukuhusu Tabianchi
Guterres ameongeza kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi zinalingana na tahadhari za mara kwa mara na utabiri uliokuwa ukitolewa na wanasayansi.
Amesema kinachoshangaza tu ni kasi ya mabadiliko.
Kutokana na yote haya, Guterres ametaka hatua za haraka zichukuliwe kwa mara nyengine tena akiilenga sekta ya nishati ya visukuku.