1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takribani watu 200 wauwawa nchini Sudan

18 Aprili 2023

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa pande zinazopigana nchini Sudan kusitisha mara moja uhasama huku mjumbe wake mjini Khartoum akisema takriban watu 200 wameuawa na mapigano hayo.

Sudan Khartum Kämpfe Rauch
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema kuongezeka kwa mzozo kati ya jeshi na vikosi vya kijeshi, wakiongozwa na majenerali wapinzani kunaweza kusababisha hali mbaya kwa nchi na eneo hilo kwa ujumla.

Vurugu hizo, zilizozuka Jumamosi, ziliendelea, huku idadi ya vifo ikiongezeka na watu wasiopungua 185 wakitajwa kupoteza maisha, Volker Perthes, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, aliwaambia waandishi wa habari.

Mnyukano wa kuwania madaraka unaendelea

Mapigano hayo yalizuka baada ya wiki kadhaa za myukano wa kuwania madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021. Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi chenye nguvu cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).

Umoja wa Mataifa umesitisha shughuli zake nyingi nchini humo, alisema msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric, ambaye alisisitiza Umoja wa Mataifa hautakuwa na ulazima wa kuwahoji wahudumu wake wasipotokea maofisini kutokana na mashaka ya usalama.

Hali mbaya ya maisha kwa wakazi wa Sudan

Makao makuu ya jeshi mjini KhartoumPicha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Katika taarifa yake, mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths amesema mapigano hayo mapya yanazidisha hali ambayo tayari ilikuwa tete, na kulazimisha mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika weo katika huduma za kiutu  kufunga kwa muda programu zao zote zaidi ya 250 kote Sudan.

Aliongeza kwa kusema athari za kusimamishwa huko zitaonekana mara moja, haswa katika maeneo ya ambayo hali ya uhakika wa chakula na msaada wa lishe imekuwa duni, katika nchi ambayo watoto milioni 4 na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wapo katika mazingira magumu.

Mkutano wa dharura wa Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa faragha kuhusu hali nchini Sudan Jumatatu asubuhi. Wajumbe watatu kutoka matiafa ya Afrika katika baraza hilo Ghana, Gabon na Msumbiji  walitoa taarifa ya pamoja kufuatia mkutano huo, wakitaka "kusitishwa mara moja kwa mapigano."

Nchi hizo zilitoa wito kwa jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF kutumia kipindi cha mfngo wa mwezi wa Ramadhani, kubeba dhima ya suluhisho la amani na mazungumzo jumuishi ili kutatua tofauti zao.

Awali Guterres alisema kwamba mwishoni mwa juma alizungumza na viongozi hao wawili wa Sudan na anashirikiana nao  kikamilifu na Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiarabu na viongozi kote kanda katika utatuzi wa mzozo.

Uvamizi wa balozi wa Umoja wa Ulaya mjini Khartoum

Katika muendelezo wa vurugu hizo Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulkaya Josep Borell amesema Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa Sudan amevamiwa katika makazi yake mjini Khartoum. Kupitia ukurasa wake wa Twetter mwanadiplomasia huyo ameandika hatua hiyo ni ukiukwaji mkubwa wa makataba wa Vienna.

Soma zaidi:Watu zaidi ya 100 wauawa Sudan

Amesema usalama wa majengo ya kidiplomasia na wafanyakazi wake ni jukumu la msingi la mamlaka ya Sudan na wajibu chini ya sheria za kimataifa. Ingawa hata hivyo baadaye ofisi ya mwanadiplomasia huyo mwenye umri wa miaka 58, Aidan O'Hara ilisema alinusurika baada ya mkasa huo.

Chanzo: AFP