1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres ataka silaha za nyuklia zitokomezwe

11 Oktoba 2024

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatolea mwito viongozi wa ulimwengu kuzitokomeza silaha zote za nyuklia, ambazo amezitaja kama vifaa vya mauaji.

UN Generalsekretät Antonio Guterres
Picha: William Volcov/ZUMA Press Wire/picture alliance

Mwito huo wa Guterres umetolewa baada ya kundi moja la Kijapan la manusura wa bomu la wakati wa vita vya pili vya dunia, huko Hiroshima na Nagasaki, kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka huu, hii leo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema washindi hao wa tuzo ya amani ya Nobel wa kundi la Hibakusha, ni mashahidi wa ukatili uliofanyiwa binadamu kwa kutumia silaha za nyuklia.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen nae amesema kutolewa kwa tuzo hiyo kwa vuguvugu la Nihon Hodankyo au Hibakusha, ni hatua inayotuma ujumbe mzito. Kamati ya tuzo ya Nobel, imelitunuku kundi hilo kutokana na harakati zake za kupinga silaha za nyuklia.