Guterres atoa mwito wa usitishwaji wa mapigano Sudan
28 Oktoba 2025
Matangazo
Mwito wa Guterres unatolewa baada ya wanamgambo wa RSF kuuteka mji wa El Fasher jana Jumatatu. Katika taarifa, msemaji wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephan Dujarric, amesema Guterres analitaka jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF kuwasiliana na mjumbe wake wa Sudan Ramtane Lamamra,haraka kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka za kufikia makubaliano.
Wakati huo huo, Umoja wa Afrika umelaani visa vya ''Ukatili'' na "uhalifu wa kivita" vinavyoripotiwa huko El Fasher.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya umoja huo, Mahmoud Ali Youssouf kupitia taarifa aliyoitoa kwenye mtandao wa kijamii wa X, amesema ana wasiwasi kuhusu machafuko na madai ya mauaji ya kikabila yanayoendelea huko El Fasher.