1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Niger isaidiwe kukabiliana na makundi ya jihadi

Hawa Bihoga
3 Mei 2022

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitolea mwito jumuia za kimataifa kuwekeza katika kulisaidia taifa la Niger kwa ajili ya kupambana na makundi ya watu wenye itikadi kali.

UN-Generalsekretär António Guterres
Picha: Bruce Cotler/ZUMA /picture alliance

Guterres alisema jumuia za kimataifa zinatakiwa kuwekeza kikamilifu kwenye mafunzo pamoja na vifaa kwa kijeshi nchini Niger.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifaaliitembelea Niger ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika Magharibi.

Hoja ya kutetereka kwa hali ya usalama katika ukanda wa Sahel unaosababishwa na mashambulizi ya mara kwa mara na  vikundi vya jihadi inaibuka katika mazungumzo ya Rais wa taifa hilo la Afrika Magfharibi Mohamed Bazoum  pamoja na mgeni wake Katibu mkuu Guterres.

Soma zaidi:UN yaelezea hofu juu ya vurugu katika kanda ya Sahel

Alisema anaamini kwa kutazama utendaji kazi wa jeshi la nchi hiyo iliopo katika ukanda wa Sahel, Jumuia ya Kimataifa inapaswa kuwekeza kikamilifu ili kuimarisha uwezo wa jeshi, kwa kutoa mafunzo kadhalika vifaa.

Alisisitiza kwa kuzigeukia jumuai za Afrika ikiwemo Umoja wa Afrika na Jumuia ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, kwa kusema  Niger haiwezi kukabiliana na changamoto nyingi peke yake.

Guterres: Ugaidi ni tishio la kimataifa

Alisema Niger inapokabiliana na tatizo la ugaidi, inapaswa kila taifa liunge mkono sababu tatizo hilo si na nchi hiyo pekee au Afrika."jumuia za kimataifa lazima zitambue hili ni tishio la kimataifa"

Askari jeshi akiwa katika majukumu yake huko SahelPicha: Philippe De Poulpiquet/MAXPPP/dpa/picture alliance

Liahidi kuendeleza harakati za kukabiliana na tatizo hilo kama alivyoanzatangu alipokuwa katibu mkuu

"Nitahakikisha kuhamasisha upatikanaji wa nyenzo zaidi kwa ajili kukabiliana na changamoto hizi."

Hata hivyo Guterres amekiri kwamba  mataifa matano ya ukanda wa sahel ambayo inaileta pamoja Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger na Chad, yamedhoofishwa na mapinduzi ya kijeshi yaliotokea katika baadhi ya mataifa jirani.

Soma zaidi:Watu 18 wauwawa katika shambulio Sahel

kauli hiyo ya katibu mkuu ilimaanisha Mali na Burkina Faso katika kipindi cha miaka miwili iliopita. Amesema amani na utulivu nchini Niger na eneo zima  la Sahel ni kipaumbele cha juu cha Umoja wa Mataifa na kurejea  wito wake wa rasilimali zaidi ili kukabiliana na tatizo hilo.

Rais Bazoum amtunuku Guterres nishani ya sifa

Kutokana na wito huo Rais wa Niger Mohamed Bazoum amemtunuku Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa Nishani ya Sifa kutokana na kutambua dhamira yake ya kutafuta suluhu ya tatizo la Ugaidi.

Rais wa Niger Mohamed BazoumPicha: Gazali Abdou/DW

Nchi kadhaa za Magharibi zinaiunga mkono Niger katika mapambano yake dhidi ya makundi yenye uhusiano na Al-Qaeda na dola ya Kiislamu, hususan Ufaransa na Marekani, ambayo ina kambi za kijeshi huko Niamey na eneo la Agadez kaskazini.

Soma zaidi:Vikosi vya Ufaransa vyamuuwa mkuu wa IS ukanda wa Sahel

Wakati huo huo, Rais wa zamani wa Niger, Mahamadou Issoufou, amekubali ombi la Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuongoza tathmini ya Mkakati ya Umoja wa Afrika  na Umoja wa Mataifa kuhusu usalama katika Sahel, kuhusu jinsi ya kuimarisha mwitikio wa jumla wa kimataifa katika  mzozo wa usalama kwenye ukanda huo.