1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Usalama wa chakulaItaly

Guterres:Zaidi ya watu milioni 780 wanateseka kwa njaa

24 Julai 2023

Mkutano wa kilele wa siku tatu wa Umoja wa Mataifa umeanza leo mjini Rome kwa lengo la kukabiliana na mfumo uliovunjika wa chakula ulimwenguni ambapo mamilioni ya watu wanakufa njaa,mabilioni wakikabiliwa na unene

Antonio Guterres | UN Generalsekretär
Picha: Eskinder Debebe/UN Photo/Xinhua/IMAGO

 Mkutano huo wa mifumo ya chakula unajiri wakati kukiwa na uhaba unaoongezeka wa chakula kote ulimwenguni, huku mashirika ya Umoja wa Mataifa yakionya kuhusu ongezeko la idadi ya watu wanaoteseka kwa kiwango kikubwa cha njaa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika ufunguzi wa mkutano huo kuwa katika ulimwengu wenye chakula cha kutosha, inakasirisha kuwa watu wanaendelea kuteseka na kufa kwa njaa.

Amesema zaidi ya watu milioni 780 wanateseka kwa njaa kote ulimwenguni, hata wakati ambapo karibu theluthi moja ya chakula ulimwenguni kinaharibiwa au kupotea.

Soma pia:UN yahofia mzozo wa chakula Sahel

Amesema watu milioni 462 wana uzito hafifu na bilioni mbili ni wanene kupindukia.

Mkutano huo unayaleta pamoja wawakilishi watatu kutoka mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yenye makao yao makuu mjini Rome, Shirika la Chakula na Kilimo - FAO, Shirika la Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo na Maendeleo- IFAD na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani - WFP, pamoja na wakuu wa nchi, wawakilishi wa serikali na wajumbe. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW