1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Guterrs: Tuongezeni juhudi kukabili mabadiliko ya tabia nchi

28 Novemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa viongozi wa dunia kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi wakati watakapokusanyika katika mkutano wa COP28.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Mark J. Sullivan/Zumapress/picture alliance

Guterres ametahadharisha kuwa "dunia imenaswa katika mzungumko mbaya" na kuwahimiza viongozi kuchukua hatua ili kudhibiti ongezeko la joto hadi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Celcius na kuacha kutumia nishati ya visukuku.

Soma pia:Guterres ataka mkutano wa COP28 utumike kuinusuru dunia

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameyasema hayo kuelekea mkutano wa COP28 ambapo watu 70,000 wanatarajiwa kuhudhuria mkusanyiko mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa.

Wapatanishi wa kitaifa katika mkutano huo watakabiliana na masuala kadhaa ikiwemo mustakabali wa nishati ya visukuku, usaidizi wa kifedha kutoka kwa mataifa tajiri wachafuzi wa mazingira kwenda kwa mataifa masikini yanayoathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW