1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuyana

Guyana yakataa kujadiliana suala la mipaka na Venezuela

13 Desemba 2023

Rais Irfaan Ali wa Guyana amesema yuko tayari kwa majadiliano yoyote na mwenzake wa taifa jirani la Venezuela, isipokuwa madai ya Caracas ya kutwaa mkoa wa mpakani wenye utajiri wa mafuta.

Rais Irfaan Ali wa Guyana.
Rais Irfaan Ali wa Guyana.Picha: Lenin Nolly/NurPhoto/picture alliance

Akiandika kwenye mtandao wa X, rais huyo amesema suala hilo litaamuliwa na Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ).

Ali na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela watakutana siku ya Alkhamis (Disemba 14), katika visiwa vya Mtakatifu Vincent na Grenadine kwa mualiko wa waziri mkuu wa visiwa hivyo, Ralph Gonsalves.

Soma zaidi: Guyana yaomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Tarehe 3 Disemba, Venezuela iliitisha kura ya maoni juu ya udhibiti wa mkoa wa Essequibo, ambapo wapigakura waliamua mkoa huo ni miliki ya nchi hiyo.

Mwaka 2015, kampuni ya mafuta ya ExxonMobil iligunduwa kuwa mkoa huo una kiwango kikubwa kabisa cha akiba ya mafuta ulimwenguni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW