1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haaland ang'aa mechi yake ya kwanza Dortmund

20 Januari 2020

Borussia Dortmund wanaishikilia nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga kwa sasa ingawa mchezaji wao mpya waliyemsajili katika dirisha hili dogo la uhamisho la mwezi Januari Erling Haaland aling'aa

Bundesliga FC Augsburg - Borussia Dortmund | Tor Erling Haaland
Picha: AFP/T. Kienzle

Kung'aa kwa Haaland ni jambo litakalowapa matumaini ya kuweza kukwea katika jedwali na kupigania ubingwa msimu utakapokuwa unaelekea mwisho.

Katika mechi yake ya kwanza ambapo hao BVB walikuwa wanachuana na Augsburg ugenini, Haaland alipachika wavuni magoli matatu baada ya kuingia katika kipindi cha pili kama mchezaji wa akiba na kuisaidia hiyo timu yake mpya kupata ushindi wa mabao matano kwa matatu ambapo Jadon Sancho na Julian Brandt pia walicheka na wavu. Raia huyo wa Norway mwenye umri wa miaka kumi na tisa alijiunga na Dortmund kutoka RB Salzburg.

Katika mechi zengine Bayern Munich waliebuka washindi wa nne bila walipocheza na Hertha Berlin kisha bayer Leverkusen wakapata alama tatu za rahisi kwa kuwalaza Paderborn nne moja.

Vinara RB Leipzig waliwalemea Union Berlin tatu moja huko Red Bull Arena na FC Cologne wakapata ushindi kama huo huo walipokuwa wanachuana na Wolfsburg.

Sasa Leipzig ndio wanaoongoza ligi wakiwa na pointi arubaini kisha Bayern Munich wamekuja hadi katika nafasi ya pili na pointi thelathini na sita wakifuatwa na Borussia Moenchengladbach wenye pointi thelathini na tano na Dortmund wanaishikilia nafasi ya nne pointi zao zikiwa thelathini na tatu kisha tano bora inafungwa na Schalke wenye pointi thelathini na tatu pia ila wamedunishwa na uchache wa magoli ndio maana wanaishikilia nafasi ya nne.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW