1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hadhara kuu ya yaidhinisha mageuzi ya Umoja wa Mataifa

23 Septemba 2024

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeidhinisha kwa kauli moja mpango wa mageuzi ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili mjini New-York mwanzoni mwa mkutano wa kila mwaka wa hadhara kuu ya Umoja huo.

Mkutano wa baraza kuu la UN  New York
Hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa NewYorkPicha: Bianca Otero/ZUMA Wire/IMAGO

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeidhinisha kwa kauli moja mpango wa mageuzi ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili mjini New-York mwanzoni mwa  mkutano wa kila mwaka wa hadhara kuu ya Umoja huo.

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Philemon Yang ametangaza kuidhinishwa kwa mkataba huo wa Umoja wa Mataifakuhusu mustakabali wa baadae,licha ya kupingwa na Urusi na mataifa mengine mengi.

Mpango huo unakuja katika kiwingu cha kuwepo mgawanyiko mkubwa miongoni mwa jamii ya ulimwengu. Ilipangwa kwamba makubaliano hayo yataidhinishwa kwa kauli moja na nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa bila ya kupigiwa kura.

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Wassili NebensjaPicha: Michael M. Santiago/Getty Images

Hata hivyo baada ya mazungumzo yaliyoendeshwa kwa kipindi cha miezi kadhaa,Urusi ilionesha kusababisha mivutano kabla ya mkutano huo wa kilele wa siku mbili.Kwahivyo nchi wanachama wameuidhinisha mpango huo licha ya  Urusi kulazimisha ufanyike mchakato wa kupigwa kura kuhusu kile kinachoitwa mkataba wa mustakabali wa baadae.Soma pia: Marekani yaunga mkono viti viwili vya kudumu vya Afrika kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Urusi pamoja na Belarus na Nicaragua awali zilishatishia kujitenga na hatua ya kuidhinisha mpango huo katika mkutano huu wa kilele wa Jumapili,kwa mujibu wa wajumbe wao.

Mkataba kuhusu mustakabali wa Umoja wa Mataifa ulijadiliwa chini ya uongozi wa Ujerumani na Namibia,na Kansela Olaf Scholz atahutubia hadhara kuu katika ufunguzi wa mkutano huo wa kilele leo Jumapili.Hadhara kuu ya UN yaidhinisha mkataba wa mageuzi ya Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa UN-Antonio Guterres Picha: BEN MCKAY/AAP/IMAGO

Kiongozi huyo wa Ujerumani yuko NewYork licha ya kufanyika uchaguzi muhimu wa jimbo la Brandenburg ambako waangalizi wanasema, ndani ya Ujerumani na nje unafuatiliwa kwa karibu kuona ikiwa chama chake cha SPD kitakuwa na matokeo gani na hasa baada ya ushindi wa chama cha siasa kali katika majimbo ya Thuringia na Saxony yaliyofanya uchaguzi hivi karibuni.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitowa mwito wa kufanyika mageuzi katika tasisi hiyo ya Kimataifa pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ili kuifanya Jumuiya ya Kimataifa kuwa na uwezo zaidi wa kuchukuwa hatua katika kukabiliana na migogoro mingi na vita na kuufanya ulimwengu kuwa mahala pa haki.

Mkataba uliopitishwa unajumuisha maazimio yanayodhamiria kuleta mageuzi katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na kurekebishwa kwa taasisi za mifumo ya fedha ya Kimataifa,kuyapa nafasi kila kinachoitwa mataifa ya Kusini mwa dunia au mataifa yanayoendelea.