1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa baada ya jengo kuanguka yafikia 13

18 Novemba 2024

Idadi ya watu waliokufa kufuatia mkasa wa kuporomoka kwa jengo mjini Dar es Salaam nchini Tanzania imefikia 13 na zaidi ya watu 80 wameokolewa.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokufa baada ya jengo kuanguka imefikia 13Picha: Ericky Boniphace/AP/picture alliance

Hayo yamesemwa na rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan.

Jengo hilo la ghorofa nne katika soko kuu la Kariakoo liliporomoka mwendo was aa tatu asubuhi siku ya Jumamosi.

Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Samia Suluhu alisema manusura waliookolewa wamekimbizwa katika hospitali na kwamba 26 walikuwa bado wamelazwa.

Samia alisema serikali itasimamia gharama za matibabu na itasaidia kwenye mipango ya mazishi.

Majengo huporomoka katika baadhi ya miji ya Afrika kwa sababu ya viwango duni vya ujenzi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW