1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Hafla ya kuapishwa Trump kufanyika ndani ya jengo la Bunge

18 Januari 2025

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hafla ya kuapishwa kwake itafanyika ndani ya jengo la bunge la Capitol, kutokana na hali ya baridi kali inayotarajiwa huko Washington Jumatatu ya Januari 20.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari
Rais mteule wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habariPicha: Scott Olson/Getty Images

Hii itakuwa ni mara ya kwanza katika muda wa mikaa 40 kuchukuliwa kwa uamuzi kama huu wa kuhamisha  tukio hili muhimu la kidemokrasia kufanyika ndani kuliko nje kama ilivyozoeleka.

Rais wa mwisho kuapishwa ndani ya jengo ilikuwa Rais Ronald Reagan mnamo mwaka 1985 alipokula kiapo kuanza muhula wake wa pili.

Hafla ya kuapishwa kwa Trump itahudhuriwa na viongozi mbalimbali. Hata hivyo Trump amesema kuwa sherehe zingine zote zitafanyika kama ilivyopangwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW