1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hailemariam awasili Cairo kwa mazungumzo ya mto Nile

17 Januari 2018

Hailemariam Desalegn kujadili mradi wa bwawa kubwa linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile ambalo Misri inahofia kwamba litachukua sehemu yake ya mto huo

Äthiopien kündigt Freilassung politischer Gefangenen an | Hailemariam Desalegn
Desalegn
Picha: picture alliance/AA/E. Hamid

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amewasili mjini Cairo kwa ziara ya siku mbili kujadili ujenzi wa bwawa kubwa linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile na ambalo Misri inahofia kwamba litachukua sehemu yake ya mto huo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema leo katika taarifa yake kwamba Desalegn atakutana na Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi kesho, na kwamba mawaziri wa kigeni wa mataifa hayo mawili walikutana kabla ya ziara hiyo.

Misri imekuwa ikionesha wasiwasi juu ya ujenzi wa bwawa hilo ambalo linaelekea kukamilika karibuni. Mto Nile ni chanzo cha maji safi kwa idadi jumla  ya watu milioni 95 wa Misri.

Ethiopia ambayo ina idadi sawa na hiyo, imesema bwawa hilo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yake.