Ujumbe wa Haiti uko Kenya kujadili juu ya kutumwa kwa askari
14 Desemba 2023Mkurugenzi mtendaji wa polisi wa taifa wa Haiti, Frantz Elbe, na ujumbe wake uliwasili Nairobi siku ya Jumanne kwa ziara ya siku tatu, kwa mujibu wa taarifa ya afisi ya Inspekta mkuu wa polisi,Japheth Koome.
Duru zinaeleza kuwa ujio huo ni baadhi ya maandalizi ya kikosi cha maafisa alfu moja wa Kenya kujiunga na wenza wao alfu tatu watakaoshika doria mjini Port-Au-Prince chini ya mwamvuli wa ujumbe wa pamoja wa kuimarisha usalama, MSS, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Soma pia:Kenya yasema haitopeleka askari Haiti hadi Umoja wa Mataifa utoe fedha
Maafisa wanasema kuwa Kenya itapeleka kikosi cha kwanza cha maafisa 300 wa polisi nchini Haiti ifikapo Februari kama sehemu ya Ujumbe wa Kimataifa wa Kusaidia Usalama unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Mahakama ya Kenyaitatoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga kutumwa mnamo 26 Januari 2024.