1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Haiti: Polisi waua wanachama 28 wa genge la uhalifu

20 Novemba 2024

Polisi kwa kushirikiana na makundi ya kiraia ya kujihami nchini Haiti, wamewaua watu 28 wanaodaiwa kuwa wanachama wa genge la uhalifu katika mji mkuu Port-au-Prince.

Port-au-Prince | Polisi wa Haiti wakiwa katika doria
Polisi wa Haiti wakiwa katika doria mjini Port-au-PrincePicha: Clarens Siffroy/AFP/Getty Images

Polisi waliendesha oparesheni ya usiku kucha katika kitongoji cha Petionville na kulilenga kundi la Viv Ansanm linaloongozwa na Jimmy Chérizier.

Serikali inajaribu kurejesha udhibiti wa mji huo wenye vurugu na machafuko ambao kwa asilimia 80 unadhibitiwa na magenge hayo.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesema linasitisha kwa muda shughuli zake katika mji mkuu wa Haiti kutokana na kile walichosema ni vurugu na vitisho kutoka kwa polisi,  ikiwa ni zaidi ya wiki moja baada ya wagonjwa wawili kupigwa risasi na kuuawa.