1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haiti yaisifia kazi ya polisi kutoka Kenya

4 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kikosi cha polisi wa Kenya kilichotumwa hivi karibuni nchini kwake kitasaidia sana kwenye kuyadhibiti magenge yenye silaha.

Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille.
Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille.Picha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Cornille alisema siku ya Jumatano (Juni 3) kwamba askari hao wangelisaidia pia kuisogeza nchi hiyo ya Karibiki kwenye uchaguzi wa kidemokrasia, huku akikisifia kikosi hicho kwa kazi ambayo kimekuwa kikiifanya tangu kilipowasili.

Soma zaidi: Kikosi cha pili cha ujumbe wa polisi kuwasili Haiti ndani ya wiki chache zijazo

Waziri Mkuu huyo alisema kwamba sasa serikali yake itajikita kwenye kulishughulikia kikamilifu suala la ghasia za magenge na upungufu wa chakula, kuhakikisha uchaguzi huru kupitia mageuzi ya kikatiba na kisiasa na kurejesha upya imani ya umma kwa jeshi la polisi.

Mnamo tarehe 25 Juni, kikosi cha kwanza cha polisi 200 kutoka Kenya waliwasili mjini Port-au-Prince. Kenya imeahidi kutuma askari wake 1,000 wakiwa sehemu ya kikosi cha polisi wa kimataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW