1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haiti yakubali kupokea kikosi cha askari wa Kenya

31 Julai 2023

Haiti imelikubali kwa shauku kubwa pendekezo la Kenya kuongoza kikosi cha kimataifa cha askari 1,000 ili kuimarisha usalama katika nchi hiyo ya Caribbean inayokumbwa na ghasia.

Sicherheit in Haiti
Picha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Haiti, Jean Victor Geneus, ilisema kuwa Haiti inathamini nia ya mshikamano wa Afrika na inatazamia kuukaribisha ujumbe unaopendekezwa na Kenya.

Kenya ilitangaza siku ya Jumamosi (Julai 29) kuwa ilikuwa tayari kupeleka maafisa 1,000 wa polisi ili kusaidia kutoa mafunzo na msaada kwa wenzao wa Haiti katika kupambana na magenge ya wahalifu ambayo yamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mji mkuu, Port-au-Prince.

Soma zaidi: Kenya iko tayari kupeleka kikosi kusaidia kurejesha utulivu Haiti
Guterres atolea wito jamii ya kimataifa kuisaidia Haiti

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, Alfred Mutua, alisema Kenya ingeliutuma ujumbe wa kutathmini hali ilivyo nchini Haiti katika wiki chache zijazo.

Pendekezo hilo la kuisaidia Haiti bado linatakiwa kukubaliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa na mamlaka za ndani. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW