Haiti yaomba msaada wa kukabiliana na vurugu za magenge
26 Septemba 2025
Matangazo
Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Saint-Cyr, amesema hatua za haraka zinahitajika kwa sababu watu wanakufa kila siku nchini Haiti.
Saint-Cyr ameongeza kuwa ni muhimu kusema kuwa Haiti inakabiliwa na vita kati ya wahalifu wanaotaka kulazimisha vurugu kama utaratibu wa kijamii na watu wenye silaha wanaopigania utu na uhuru wa binadamu.