Haiti yaomba uchunguzi wa kimataifa kwa mauwaji ya Moise
6 Agosti 2021Taarifa ya ubalozi huo kwa taifa jirani na Haiti katika barua yake ya Agosti 3, ambayo imeelekzwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres inasema Haiti imetoa wito wa kuundnwa kamisheni maalumu ya uchunguzi pamoja na mahakama maalumu ya kuwashtaki washukiwa wa mauwaji hayo.
Katika barua hiyo ambayo imesainiwa na waziri wa mambo ya nje Claude Joseph, inaeleza Haiti inalitazama shambulio la Moise katika makazi yake, ni kama uhalifu wa kimataifa, kutokana na kuhusika kwa raia wa kigeni katika kupanga, kufadhili na kutekeleza.
Tuhuma za wanajeshi wa nje ya taifa hilo ndio msingi wa uhalifu wa kimataifa
Hadi wakati huu serikali ya Haiti imewakamata wanajeshi wa zamani wa Colombia, ambao inadaiwa walikodiwa na kampuni mmoja ya usalama ya mjini Miami, Marekani. Taifa hilo pia limeongeza muundo wa mpango huo wa uungwaji mkono ufanane na ule wa uchunguzi wa shambulizi la kigaidi la Lebanon wa 2005, ambalo lilisababisha vifo vya watu 22, akiwemo waziri mkuu.
Katika hatua nyingine ndani nchini Haiti, serikali imeimarisha usalama kwa watumishi wa mahakama wakati ikijiandaa kumtangaza jaji ambae atasimamia kesi zinazoyahusu mauwaji ya Rais Jovenel Moise. Mmoja kati ya mahakimu waandamizi wa asasi yenye dhamani ya kuwateuwa majaji ya kuendesha kesi hiyo ya Port-au Prince Bernard Vil, anasema hatua hiyo inatokana na wasiwasi wa kiusalama wa wahudumu wa sekta hiyo.
Baadhi ya majaji wanahofu ya kushiriki kesi ya Moise kwa usalama wao
Amesema baadhi ya majaji ambao amewasilianao nao katika siku za hivi karibuni kuhusu kesi hiyo, wamemweleza kwamba wanawasiwasi na usalama wao. Lakini yeye amaesema hana wasiwasi katika wakati huu wa jukumu la kuamua nani apewe dhamana. Aidha ameongeza kusema tabia ya mwanzo ya hakimu ni ujasiri, kwa sababu hakimu anapaswa kufanya maamuzi.
Pia mwanasheria huyo alisema mamlaka inafahamu uhitaji wa nyongeza ya ulinzi inahitajika, kwa vile wapo baadhi ya maofisa wengine wa mahakama wamekwenda mafichoni kutokana na kuwepo kwa vitendo vya kutishiwa kuuwawa. Makarani wa mahakama imeripotiwa kupokea vitisho vinavyowalazimisha wayafanyie marekebisho majina na maelezo ya ripoti ya mauawji ya Julai 7 ya Rais Moise, tukio ambalo lilisababisha pia kujeruhiwa vibaya kwa mkewe.
Vyanzo: RTR/AP