1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki ya elimu ni kwa wote

19 Juni 2012

Licha ya kuwa kila mwanadamu anayo haki ya kupata fursa sawa za maisha kwa sababu ya ubinaadamu wake na siyo katika msingi wa nasaba yake ya kijamii, jinsia dini au dini, lakini hali halisi ni nyingine kabisa.

Mpango wa elimu kwa wote Sudan ya Kusini.
Mpango wa elimu kwa wote Sudan ya Kusini.Picha: Angelika Mendes

Katika karne ya 18 usawa lilikuwa miongoni mwa masuala muhimu sana kwa Waliberali wa Uingereza. Watu wa tabaka la kati walikusudia kuzilinda haki zao dhidi ya mabwanyenye waliokuwa na istihaki.

Waliberali walitaka kila raia awe na haki ya kujiamulia mwenyewe juu ya njia za kuzichukua katika maisha yake. Hata hivyo, usawa wa kijamii halikuwa suala la kipaumbele. Iliwapasa wanawake waendeshe harakati hadi mwishoni mwa karne 19 ili kupata haki ya kushiriki katika maamuzi ya kisiasa katika misingi ya kidemokrasia.


Nchini Ujerumani, inapohusu wanawake kupata fursa sawa kwenye soko la ajira na kulipwa mishahara sawa na wanaume,a kina mama bado wanaendelea kupunjika.

Pia katika sekta ya elimu na mafunzo ya kazi,wasichana na wavulana hawapewi fursa sawa katika sehemu nyingi za dunia. Lakini sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linadhamiria kuibadili hali hiyo kwa njia ya kuutekeleza mpango wake unaoitwa "Elimu kwa Wote"

Mpango wa Elimu kwa Wote

Nchi 164 zimekubaliana kutoa elimu ya msingi kwa wototo wote bila ya malipo. Aidha zimekubuliana kupunguzakwa nusu hali ya kutojua kusoma na kuandika miongoni mwa watu wazima sambamba na kuhakikisha usawa wa jinsia.Kila mtu anayo haki ya kupata elimu.

Hayo ameyasema mkuu wa kitengo cha nidhamu, elimu na maendeleo endelevu wa UNESCO, Mark Richmond, ambaye anatumai kwamba kwa kadri watu watakavyosimama kidete kusisitiza haki ya elimu,ndivyo serikali zitakavyoitilia maanani haki hiyo na kuiingiza katika sheria za nchi.

Hata hivyo, haki ya elimu siyo jawabu la kila swali. Katika nchi nyingi tajiri za viwanda kila mtoto anawajibika kuenda shule na kwa hivyo, kila mtoto anayo haki ya kupata elimu ya msingi.

Paul Rose anaesimamia ripoti za kila mwaka juu ya maendeleo ya elimu zinazotolewa nya shirika la UNESCO amesema ingawa idadi ya watoto wanaokwenda shule inaongezeka, bado wapo watoto milioni 67 ambao hawaendi shule.

Nchini Ujerumani elimu ya hadi kidato cha sita kwenye shule za serikali inatolewa bila ya malipo.Kila mtoto anayo fursa ya kumaliza masomo yake kwa kufanya mtihani wa kumwezesha kuingia chuo kikuu.

Katika nchi zinazoendelea aghalabu ufisadi na umasikini unazuia juhudi za kutoa fursa sawa za elimu.Familia za masikini hazina mapato ya kuwawezesha kulipa ada za watoto, achilia mbali kununua vitabu na sare kwa ajili ya watoto.

Mwandishi: Gaby Reucher/DW
Tafsiri: Abdu Mtullya
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW