Haki za binadamu China.
26 Februari 2009Matangazo
WASHINGTON.
Marekani imeilaumu China, vikali kwa kukiuka haki za binadamu , wiki moja baada ya waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton kufanya ziara nchini China ambapo hakusema kitu juu ya suala hilo
Katika ripoti yake ya kila mwaka juu ya haki za binadamu duniani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imeilaumu Urusi ambako imesema haki za raia zinabanwa.
Lakini China imesema kuwa ripoti hiyo haina msingi.
Ripoti hiyo pia inatilia maanani mfumuko wa sheria zinazoyabana makundi yasiyo ya kiserikali katika sehemu mbalimbali za dunia.