1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Hakimu aliyepigwa risasi mahakamani nchini Kenya afariki

15 Juni 2024

Hakimu mmoja nchini Kenya aliyepigwa risasi na polisi wakati akiendesha kesi mahakamani amefariki. Hayo yametangazwa leo na Jaji Mkuu Martha Koome.

Nairobi, Kenya | Jaji Mkuu Martha Koome.
Jaji mkuu Kenya Martha Koome. Picha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Monica Kivuti, hakimu katika mahakama ya Makadara mjini Nairobi, alipigwa risasi Alhamisi baada ya kukataa ombi la kumuwachia kwa dhamana mke wa afisa huyo wa polisi.

Polisi huyo kisha alipigwa risasi na kuuawa na polisi wenzake. Katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa X, Koome amesema Kivuti amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata. 

Soma pia:Mahakama Kenya yaongeza amri ya kuzuia polisi kupelekwa Haiti

Maafisa watatu wa polisi pia walijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo lakini Koome hajatoa habari kuhusu hali yao.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW