Hakuna makubaliano ya tarehe ya uchaguzi Mali
21 Machi 2022Kimsingi kunaelezwa kwa watawala wa kijeshi kwa sasa, ambao ulilichukua taifa hilo kwa mtutu wa bunduki Agosti 2020 ungetaka kudumu madarakani kwa muda usiopindukia miaka minne. Hayo ni kwa mujibu wa chanzo kimoja nchini Mali, ambacho kilizungumza na Shirika la habari la AFP, pasipo kutoa ufafanuzi zaidi.
Ziara ya siku mbili ya Jonathan ilikuwa la lengo mahususi la kupata muafaka juu ya tarehe ya uchaguzi, baada ya kusema kuwa miaka mitano inayozungumziwa ni kipindi kirefu mno. Na baada ya utawala wa kijeshi katika mkutano wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS wa Accra, Ghana wa mwezi uliopita pia kupendekeza miaka minne.
Hakuna hatua zilizopigwa katika mkutano
Chanzo cha karibu na mazungumzo hayo, akitajwa kuwa mjumbe katika ujumbe wa Rais Jonathan, kilisema kwa msisitizo kwamba wamehitimisha mkutano wao wa Bamako, na kwa yeyote anaetaka kujua kama wamefikia makubaliano anasema moja kwa moja hapana. Awali kabisa kabla ya ziara yake hii ya sasa, Jonatahan aliuelezea utawala wa kijeshi kuwa usiokubalika, kwa sababu haukupitia mchakato wa uchaguzi na umewekewa vikwazo vikali na ECOWAS mwezi Novemba mwaka uliopita.
Lakini pia mapema mwaka huu ECOWAS na Umoja wa Ulaya zilimwekea vikwazo waziri mkuu wa mpito wa Mali pamoja na maafisa wa karibu na rais wa mpito Assimi Goita, baada ya kitendo cha jeshi kuvuruga mpango wa uchaguzi uliopaswa kufanyika Februari.
Uchaguzi wa Mali ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 16
Waraka wa ECOWASambao AFP iliipata nakala yake, unapendekeza uchaguzi wa Mali ufanyike katika muda wa kati ya miezi 12 na 16 kuanzia sasa, chini ya usimamizi wa tume huru ya uchaguzi.
Mali imekumbwa na kadhia za mapinduzi ya kijeshi katika awamu mbili tofauti ndani ya miaka miwili iliyopita.
ya mwanzo ilikuwa Agosti 2020 na kisha ya pili Mei 2021 ambayo Kanali Goita alifanywa rais wa mpito. Hali hiyo imeiathiri Mali, moja kati ya mataifa masikini zaidi duniani, ambalo hali yake ya usalama umekuwa ukichagizwa na muongo mmoja wa uasi kutoka kwa makundi ya waasi na wenye itikadi kali katika eneo la kaskazini mwa taifa hilo.
Vyanzo: AFP/RTR