Hakuna waliofika Ujerumani chini ya sheria mpya ya wakimbizi
26 Oktoba 2025
Matangazo
Serikali ilisitisha haki ya watu wenye hadhi ya ulinzi wa muda, kuwaleta ndugu zao kwa miaka miwili, ikidai ni kupunguza mzigo kwa mifumo ya mapokezi na ujumuishaji.
Ingawa kigezo maalum cha kiubinadamu kilianzishwa kuruhusu wenzi na watoto wadogo kuungana na wapokeaji katika visa vya kipekee, hakuna aliyewasili hadi sasa.
Kila kesi inakaguliwa kwa usaidizi wa Shirika la Uhamiaji la Kimataifa kabla ya kuwasilishwa Wizara ya Mambo ya Nje.
Mbunge Clara Bünger kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha die Linke, amesema masharti hayo ni magumu mno, na kwamba serikali "inazitenganisha familia za wakimbizi,” huku mashirika ya misaada yakihofia kuhimiza maombi mapya kutokana na vigezo vizito.